Tiote afariki

R.I.P Tiote 
Mchezaji wa zamani wa Newcastle United, Cheick Tiote,30,aanguka na kufariki huko nchini nchina.
Tiote alianza kucheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht,huku akiwahi kuichezea Roda fc kwa mkopo.
Baada ya hapo alielekea nchini Uholanzi aliichezea FC Twente mara 86,na kujiwekea sifa kama kiungo mkabaji hodari.
Baadae mwaka 2010 alijiunga na Newcastle ya uingereza akiichezea mara 150,na iliposhuka daraja alielekea nchini China mwanzo wa msimu wa 2016-17.
Alijiunga na Beijing Enterprise na ameichezea mechi 17 kabla ya kukutana na kifo chake.
Mchezaji mwenzake wa zamani wa Newcastle, Demba Ba alikuwa miongoni mwa Wachezaji wa mwanzo kutuma rambirambi zao Kupitia mtandao wa Twitter.
"May Allah grant you Jannah brother Tiote," aliandika Demba Ba.
Jonas Gutierrez naye aliandika,"Very sad to hear about the pass away of brother Tiote, R.IP my friend #nufc .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bellerin kuelekea Barcelona?

TETESI ZA USAJILI JUMANNE 20.6.2017

Jezi mpya ya Simba SC