Benitez kuivamia safu ya ulinzi ya arsenal


Meneja wa Newcastle united iliyopanda daraja kucheza ligi Kuu msimu huu, Rafa Benitez anawinda huduma za beki wa kushoto wa Arsenal,Keran Gibs.
Gibs aliyejikuta akisugua bench na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza huenda akaihama arsenal na kujiunga na Newcastle ili kupata muda mwingi wa kucheza. Kusajiliwa kwa beki mpya wa kushoto,  Kolasinac kutoka klabu ya shalke kumeongeza ushindani katika safu hiyo ya ulinzi na hili linaweza kuongeza chachu ya Gibbs kuihama arsenal.

 Gibbs ameanzishwa michezo 11 tu msimu huu tangu Desemba mwaka jana alipoumia. Mfumo mpya wa Wenger 3-4-2-1 umemkosesha nafasi Gibbs na Nacho Monreal amekuwa chaguo la kwanza la Meneja Arsene Wenger. Benitez anatarajiwa kujiimarisha msimu huu ili Newcastle united ibakie kwenye kwenye ligi Kuu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bellerin kuelekea Barcelona?

TETESI ZA USAJILI JUMANNE 20.6.2017

Jezi mpya ya Simba SC