Simba haina mipango na Ndikumana













Mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba, Zakariya Hanspop amekanusha habari kwamba klabu yake inanyemelea saini ya beki kisiki na nahodha wa Mbao FC ,Yusuph Ndikumana raia wa Burundi.
Ziara ya hivi karibuni ya Hanspope nchini Burundi Inaonekana kama njia ya Hanspope kufanya majadiliano na beki huyo jambo ambalo Wakala wa Ndikumana anayefahamika kama Kadito amedai kuwa ni kinyume na utaratibu. Hata hivyo Hanspope amekanusha taarifa hizo huku akidai alienda Burundi kwa sababu za kibiashara.
"Mchezaji mzuri tunamuhitaji lakini huyu Ndikumana hajakuwa kwenye mipango yetu," alisema Hanspope
Alimtupia lawama walaka huyo kuwa ameanika hadharani kile anachodai kuwa ni uzushi na yeye (Kadito) aliyemfata Hanspope kuhusiana na simba kumsajili Ndikumana.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bellerin kuelekea Barcelona?

TETESI ZA USAJILI JUMANNE 20.6.2017

Jezi mpya ya Simba SC