Klabu 5 ambazo Diego Costa anaweza kuamua kujiunga na moja kati ya hizo
Muhispania huyo amewaambia waandishi wa habari kwamba meneja Antonio conte amemtumia ujumbe kkuwa hana mipango naye msimu ujao.
Mshambuliaji huyo matata amewaeleza wanahabari nchini Uhispania kwamba meneja Antonio conte amemtumia ujumbe kwamba hana mipango naye msimu ujao.Aliyasema haya wakati nchi yake ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Colombia siku ya Jumatano.
Je costa Ataelekea wapi?
Hizi hapa ni timu 5 ambazo anaweza kujiunga nazo.
1. Chinese Super League
![]() |
Costa aliwahi kuhusishwa na China mwaka jana. |
China kutamfaa zaidi costa Costa hasa ukiangalia umri unavyokwenda na mkwanja atakaopokea.Matajiri wa China wanataka kumfanya Costa awe mchezaji anaepokea Mshahara mkubwa duniani.
Je Costa Costa atafuata mpunga china?
2. Atletico Madrid
Amehusishwa na klabu yake ya zamani Atletico Madrid lakini klabu hiyo kwa sasa imepigwa marufuku ya kutosajili mchezaji yoyote mpaka mwaka ujao,hata hivyo anaweza kutia saini na klabu hiyo lakini ajiunge nao mwezi Januari mwaka ujao.
Je Costa ana thamani ya kusajiliwa na Diego Simione?
3. Manchester United
![]() |
Ameshawahi kufanya kazi na Mourinho |
Lengo lao la kumsajili Antoine Griezmann linaonekana kufifia na Madrid sio rahisi kumuachia Alvaro Morata.
Zlatan Ibrahimovic atakosekana hadi mwaka ujao kutokana na majeruhi hata kama ataamua kusalia Old Trafford.Mourinho anahitaji mshambuliaji ili kukiweka sawa kikosi chake.Mourinho na Costa wamekuwa pamoja darajani ingawa uhusiano wao baadae ulikuwa wa mashaka.
Je Costa atajiunga na Mourinho?
4. Paris Saint-Germain
![]() |
PSG wanahitaji mshambuliaji. |
Emery yupo sokoni kutafuta mshambuliaji na pesa sio tatizo kwao.
PSG imekuwa mbioni kumsajili Pierre-Emerick kutoka Borussia Dortmund lakini makubaliano hayaafikiwa.
PSG wanatafuta nguvu za kuregesha ubingwa mwakani baada ya kupokonywa taji la League 1 na Monaco msimu uliopita.Je unadhani Costa atakuwa mwokozi wao sahihi?
i
5. Inter Milan
Inter wapo mbioni kuhakikisha wanarudi katika hali yao ya zamani. Hivi karibuni klabu hiyo ilichukuliwa na matajiri wapya kutoka china na fedha sio tatizo kwao.Inter wanahitaji magoli,na Diego anahitaji kikosi cha kwanza kucheka na nyavu .
Je Diego Costa atajiunga na klabu gani msimu ujao?
Chelsea
China
Atletico Madrid
Manchester United
PSG
Inter Milan?
o
Maoni
Chapisha Maoni