Ni dhahiri shahiri kwamba kati ya timu nne zitakazocheza nusu fainali ya Sportpesa super cup, lazima timu moja kutoka Kenya itafika fainali. Kati ya Mabingwa wa zamani wa Sportpesa Premier League Gor Mahia fc na chipukizii wanaoshiriki michuano ya kimataifa kwa mara ya kwanza vijana kutoka mji wa Nakuru, Nakuru Allstars wataamua nani atakutana naye kati ya Yanga au AFC leopards.
Ni ukweli usiopingika kuwa mashindano haya yamekosa ule mvuto uliotegemewa kwa kukosekana nyota muhimu kwa kila timu. Hii siioni kuwa ni sababu ya timu zetu kufanya vibaya ila hii ni nafasi kwa chipukizi wetu hasa wazawa kuonesha viwango vyao. Ni ukweli usiofichika kwamba timu ya Azam fc pekee Ndio ina mipango ya kutilia mkazo swala la vijana kuliko zilivyo timu za simba na Yanga.
 |
Wachezaji wa Nakuru All stars wakisherehekea ushindi wao baada ya kuilaza Simba SC 5-4 katika mikwaju ya penalti.
Timu zote zilizoshiriki mashindano haya zimewakosa wachezaji wake nyota kwa sababu ya kalenda ya fifa.Timu ya taifa ya kenya ipo kambini sambamba na yetu ya tanzania. Gor Mahia imewakosa nyota wake 15 ambao 10 wote wameitwa na tumu zao taifa,AFC Leopards 8,Tusker 12 na Nakuru ni timu daraja la pili.Tumeishuhudia Yanga pia ikibahatisha juzi fhidi ya Tusker fc.Tatizo sio nani atakuwa bingwa.Suala kubwa hapa ni vipi timu zetu zinaweza kutoa ushindani mkali na timu za nje.
|
Maoni
Chapisha Maoni