KOMBE LA MABARA
Urusi yalala kwa Ureno, New Zealand yatupwa nje kombe la mabara
Wenyeji wa
michuano ya kombe la mabara timu ya taifa ya Urusi wamepoteza mchezo
wao wa pili dhidi ya timu ya taifa ya Ureno kwa bao 1-0 katika mchezo
uliochezwa katika dimba la Spartak Jijini Moscow.
Mchezaji bora
duniani Cristiano Ronaldo ndie aliyefunga goli pekee katika mchezo huo
katika dakika ya nane ya mchezo akiunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa
kutoka upande wa kushoto na Raphael Guerreiro.
Maoni
Chapisha Maoni