Steve Sidwell asaini mkataba mpya na Brighton Albion


Kiungo mwenye uzoefu Steve Sidwell asaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu yake ya Brighton & Hove Albion.

Sidwell, 34, alijiunga na Brighton kwa mara ya pili January 2016,mara ya kwanza akiwa hapo kwa mkopo akitokea Stoke City.
Meneja wa Brighton amesema," Anastahili mkataba mpya na nina furaha amesaini."
"Mashabiki wetu wanafahamu ubora wake,ana tajriba na uzoefu wa kutosha hasa katika ligi Kuu England."
Sidwell alianza kucheza soka lake la kulipa akiwa na arsenal kabla ya kujiunga na Brighton mwaka 2002/03,ambapo ndiye mchezaji mwenye uzoefu mkubwa katika klabu hiyo akiwa amecheza mechi 200 premier league akiwa amefunga mabao 21 akiwa na vilabu vya Reading, Chelsea, Aston Villa,Fulham na Stoke.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Bellerin kuelekea Barcelona?

TETESI ZA USAJILI JUMANNE 20.6.2017

Jezi mpya ya Simba SC