Stars yailaza Afrika Kusini Cosafa

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wameichapa timu ya Taifa ya Afrika kusini kwa bao 1-0 katika michuano ya kombe la Cosafa.
Bao la dakika ya 18 la mshambuliaji Elias Maguri lilitosha kuipeleka Stars katika nusu fainali ya michuano katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Royal Bafokeng, Rusternburg.
Tanzania sasa itamenyana na Zambia siku ya Jumatano katika mchezo wa nusu fainali, wakati Afrika Kusini wanaangukia kwenye michuano ya Plate, inayoshirikisha timu zilizotolewa hatua ya robo fainali.
Katika mchezo wa pili wa michuano hiyo Zimbabwe waliwachapa Swaziland kwa mabao 2-1.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jezi mpya ya Simba SC

Tetesi za usaliji barani Ulaya Jumatatu 19.6.2017

TETESI ZA USAJILI JUMANNE 20.6.2017