Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2017

CAF yatathmini kubadili tarehe ya mashindano barani Afrika

Picha
Kombe la taifa bingwa barani Afrika huenda likahamishwa hadi msimu wa joto kama sehemu ya mazungumzo yaa shirikisho la kandanda barani Afrika. Kuandaliwa mashindano hayo miezi ya Januari na Februari imeghadhabisha vilabu vya bara Ulaya ambapo wachezaji wengi wa kiafrika hucheza. Pia idadi ya timu zinashoriki huenda ikaongezwa kutoka 16 hadi 24. Wachezaji wengine walikataa ombia la kuwataka kujiunga nchi zao kushirikia mashindani ya mwaka huu, yaliyoandaliwa nchini Gabon na kuamua kubaki na vilabu vyao. Hao ni pamoja na wachezaji kadha kutoka Cameroon ambao walitaka kujiunga na timu ambayo hata hivyo ilishinda kombe hilo. Hao ni pamoja na wachezaji kadha kutoka Cameroon ambao walitaka kujiunga na timu ambayo hata hivyo ilishinda kombe hilo. Kila baada ya miaka miwoli mzo huibuka kati ya vilabu vya Ulaya na nchi, vinavyodai kuwapoteza wachezaji wakati wanahitaji sana. Kwa mujibu wa vilabu hivyo mara nyingi wachezaji hurudi vilabuni wakati wamechoka baada ya kuishiriki mechi za ...

Tetesi za usajili barani Ulaya. Jumatano 19.7.2017

Picha
Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amekubali dau la Paris Saint-Germain, baada ya klabu hiyo ya Ufaransa kuwa tayari kutoa pauni milioni 195. (Esporte) Makamu wa rais wa Barcelona Jordi Mestre amesisitiza kuwa Neymar hatoondoka Barcelona wakati wowote ule. (Star) Mtaalam wa soka wa Amerika ya kusini Tim Vickery amesema Neymar huenda akaondoka Barcelona ili kuepuka kuwa chini ya kivuli cha Lionel Messi. (BBC Radio 5 Live) Kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, anataka mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki ili kujiunga na Tottenham, huku klabu yake ya Everton ikitaka pauni milioni 50 kama ada ya uhamisho. (Mirror) Tottenham watalazimika kumlipa kiungo Moussa Sissoko, 27, ili aondoke, licha ya kutoa pauni milioni 30 kumsajili mwaka jana tu. (Daily Mail) Arsenal watajaribu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzima, 29, iwapo Alexis Sanchez, 28, ataondoka Emirates. (Don Balon) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema Alexis Sanchez, 28, anayesakwa na Manchester City, ...

Tetesi za soka barani Ulaya

Picha
Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN) Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Danny Rose, 27. (S...

Tetesi za Usajili barani Ulaya: Ijumaa 14.7.2017

Picha
Chelsea wameambiwa wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, kwa pauni milioni 60 baada ya Tianjin Quanjian ya China kusema haitaki tena kumsajili mchezaji huyo. (Daily Mail) Borussia Dortmund huenda wakaamua kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, ambaye pia anasakwa na Everton, West Ham, Marseille na AC Milan. (Daily Mirror) Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, amempigia simu meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kumuambia hana mpango wa kuondoka Chelsea msimu huu. (Diario Gol) Chelsea wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 40 kwa mkataba wa miaka mitano. (RMC) Meneja wa Chelsea anajiandaa kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwa pauni milioni 40. Matic amekuwa akifanya mazoezi peke yake na anataka kuungana na Jose Mourinho Old Trafford. (Daily Telegraph) Barcelona wanataka kumsajili beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta baada ya kushindwa kumpata Hector Bellerin wa...

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu 3.7.2017

Picha
Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 125 ili kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco na kuwazidi kete Real Madrid (Sunday Mirror). Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemuambia Alexis Sanchez, 28, kuwa hatojiunga na Manchester City msimu huu (Mail on Sunday). Everton wanapanga kutaka kutoa pauni milioni 20 kumsajili mshambuliaji wa Arsnenal Olivier Giroud, 30 (The Sun). Meneja wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ameonekana kutaka klabu yake kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwa kusema Sanchez ni "mchezaji mzuri" (London Evening Standard). Alexis Sanchez Manchester City pia wanamtaka Alexis Sanchez, lakini Arsenal hawatoruhusu mchezaji huyo kwenda katika klabu hasimu inayocheza Ligi Kuu ya England (Mail on Sunday). Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, yuko tayari kumruhusu kipa Joe Hart , 30, kuhamia kwa mahasimu wao Manchester United (Sunday Express). Meneja wa Manchester United Jose Mourinho bado atataka kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 24...

Ujerumani yatwaa ubingwa

Picha
Timu ya taifa ya Ujerumani imetwaa taji la kombe la mabara baada ya kuishinda Chile kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Saint Petersburg nchini Urusi. Mshambuliaji Lars Stindl ndie aliyeifungia Ujerumani goli pekee liliwapa ubingwa wa mabara kwa mara ya kwanza baada ya kutumia vyema makosa ya kiungo wa Chile, Marcelo Diaz. Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Ureno walifanikiwa kutwaa medali ya shaba baada ya kuichapa Mexico kwa mabao 2-1. Wachezaji wa Ureno wakishangilia Beki wa Ureno Luis Neto aliwapa Mexico goli la kuongoza baada ya kujifunga katika dakika ya 55, kabla ya Pepe kuzawazisha goli hilo katika dakika za lala salama. Bao la mkwaju wa penati lilifungwa na Adrien Silva katika dakika ya 104 likawapa Ureno ushindi muhimu licha ya kumkosa nyota wake Cristiano Ronaldo.

Stars yailaza Afrika Kusini Cosafa

Picha
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wameichapa timu ya Taifa ya Afrika kusini kwa bao 1-0 katika michuano ya kombe la Cosafa. Bao la dakika ya 18 la mshambuliaji Elias Maguri lilitosha kuipeleka Stars katika nusu fainali ya michuano katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Royal Bafokeng, Rusternburg. Tanzania sasa itamenyana na Zambia siku ya Jumatano katika mchezo wa nusu fainali, wakati Afrika Kusini wanaangukia kwenye michuano ya Plate, inayoshirikisha timu zilizotolewa hatua ya robo fainali. Katika mchezo wa pili wa michuano hiyo Zimbabwe waliwachapa Swaziland kwa mabao 2-1.